> Hii ndiyo mbinu mpya ya kusafirisha madawa ya kulevya | MAPENZI

Hii ndiyo mbinu mpya ya kusafirisha madawa ya kulevya

Tumekua tukizipata taarifa za watu mbalimbali kukamatwa na dawa za kulevya kwenye viwanja vya ndege pamoja na sehemu nyingine za kusafirishia ambapo kila mmoja amekua na mbinu yake kusafirisha mzigo huo haramu.Stori mpya ya leo imetokea Nigeria ambapo mwanaume aitwae Mama Solomon kutoka Enugu amekamatwa kwenye uwanja wa ndege Lagos akiwa ameficha dawa za kulevya aina ya Cocaine katikati ya soli ya kiatu cha Mwanamke.

Jamaa alikua akitokea Brazil ambayo ni nchi maarufu sana kwa kuziuzia nchi nyingine dawa za kulevya na alikua na mifuko miwili iliyojaa viatu vya Wanawake na pochi.
Baada ya kukamatwa, Solomon mwenye umri wa miaka 27 alikataa dawa hizo kuwa za kwake na kusema yeye amekua akifanya kazi na kuishi nchini Brazil hivyo kuna rafiki yake alimpatia huo mzigo na kumwambia akiufikisha salama atazawadiwa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top