> MAPENZI: kitaifa

Madhara yatokanayo na kusambaa kwa picha za ngono katika mitandao ya kijamii..

Mapenzi ni kitu nyeti sana katika tamaduni zetu za kiafrika, mapenzi ni kitendo cha faragha sana katika maadili ya kitanzania ambapo tunapaswa  kuheshimu, kukitunza na pia kukihifadhi sehemu husika kama vitabu vya dini vinavyosema.

Utandawazi ni kitu kipana sana kinachopaswa kutumika kwa mipaka kulingana na sheria za nchi na taratibu zilizowekwa na vyombo mbali mbali vya kisheria na kiserikali pia. Watu wengi wanajikuta wakiathiliwa na kutazama picha za ngono mitandaoni bila kujua.

Madhara ya kwanza ya kuweka picha za ngono katika mitandao yetu ya kijamii ni:-

1. kubadilisha misimamo ya kimahusiano kwa walio wengi na kujikuta ukitawaliwa na tamaa za kimwili.

2. Kuongeza kiu ya kufanya mapenzi wakati wote umuonapo mwanamke au mwanaume kwa namna moja ama nyingine akiwa amevaa nguo fupi, za kubana nk.

3. Kutoka nje ya ndoa mara kwa mara kwa wale waliooa na hata walio bado kuoa huongeza idadi ya kuwa na wapenzi tofauti tofati kulingana na tamaa yao; kwa mfano weupe/weusi, warefu/wafupi, wanene/wembamba nk kwani kile ukionacho ndicho huingia akilini.

4. Kuongeza idadi ya kufanya mapenzi zaidi ya kawaida, kitu ambacho ni hatari kwa afya zetu na kwa maendeleo ya taifa letu.

5. Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile kutokana na yale unayoyaona yakifanyika katika mitandao mbali mbali ya ngono. Jambo ambalo ni kinyume na vitabu vya dini na kisheria pia.

6. Wanafunzi wengi kuanza kufanya mapenzi wakiwa chini ya umri, kitu ambacho kuwaathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya zao.

Wanaomiliki wa website, blogs na mitandao ya kijamii kama Facebook, Folum Tweeter nk. hapa nchini tuwe wabunifu wakupata wasomaji, tukemee picha za ngono katika mitandao yetu kwani taifa la leo na kesho ni vijana na vijana wadogo.

Tazama picha hizi kali za watoto wa .COM wanavyopagawisha na utandawazi..



Seriou's na masomo au anapitia pitia Kweli huyu mtoto noooooma!!!
 
Mmmwaaaaaaaa..h''..

Hapa kazi na Dawaaaaaaa!!!

Du! hapa sina la kusema..!

Weweeeeeeeee!!!! Kweli Gambe noma! Mbona keleleeeeeeee!!!!!?

Rangi mseto!

Nini tena?!

Watu zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali ya coster Mbeya

 

Baadhi ya majeruhi wakitafuta mizigo yao mara baada ya kutoka ndani ya basi hilo


Baadhi ya majeruhi wakitoka ndani ya basi hilo
 

Baadhi ya abilia wakitaka kumpiga Dereva wagari ya aina ya Suzuki kuwa yeye ndio alisababisha ajali hiyo kwa kuyumbayumba kwake barabarani









WATU zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Costa kutoka Mbozi kuelekea Mbeya kupinduka katika eneo la  Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya.

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 336 CJY ambalo lilipinduka baada ya kumshinda dereva wakati akijaribu kulikwepa gari linguine aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 327 ARZ.

Kwa mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

Baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.

Wazazi wa Miss Tanzania,Lilian Kamazima wahoji kuhusu zawadi za mtoto wao..Soma kilichojiri hapa



Wazazi wa Miss Tanzania mpya, Lilian Kamazima wameitaka Kamati ya Miss Tanzania  hitoe maelezo ya uhakika kuhusu zawadi na taji la binti yao kwa kuwa hadi sasa wako njia-panda. Kauli hiyo ya  Eva na Deus Kamazima imekuja siku chache baada ya mrembo huyo kuwasili jijini Arusha akitokea Dar es Salaam.

Wakizungumza nyumbani kwao, Majengo Juu jijini Arusha jana, wazazi hao walionyeshwa kushangazwa na hatua ya kumpokea binti yao akiwa hana taji, pamoja na fedha ambazo alistahili kupatiwa kama mshindi.

Walisema kuwa walimpokea binti yao kama ‘yatima’, hata tiketi ya ndege alilazimika kulipiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Investment Ltd, aliyemuibua katika ngazi ya Kanda ya Kaskazini.

“Tunaiomba Kamati ya Miss Tanzania itupe maelezo ya kina kuhusu zawadi, taji pamoja na vitu vingine kwa kuwa tumempokea binti yetu kama bila zawadi wala taji,” walieleza wazazi hao kwa nyakati tofauti.

Awali, mrembo huyo alisema kuwa pamoja na kwamba bado hajakabidhiwa taji wala zawadi yoyote na Kamati ya Miss Tanzania, lakini kitendo cha kupewa kiti hicho ameridhika.

“Sijapewa taji wala zawadi , lakini kitendo cha kupewa kiti cha umalkia nimeridhika,” alisema  Lilian.

Mkurugenzi wa  Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema kuwa ni kweli bado hawajamkabidhi fedha na zawadi  kwa kuwa kuna taratibu za kiofisi bado zinafanyika.

“Ni kweli, tulimwambia atuachie akaunti yake kwa kuwa kuna taratibu zinafanyika, tutamwekea pesa na kuhusu zawadi huyo alirithi taji, hakuwa mshindi wa kwanza, lazima mwelewe,” alisema Lundega.
Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top