> Watu zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali ya coster Mbeya | MAPENZI

Watu zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali ya coster Mbeya

 

Baadhi ya majeruhi wakitafuta mizigo yao mara baada ya kutoka ndani ya basi hilo


Baadhi ya majeruhi wakitoka ndani ya basi hilo
 

Baadhi ya abilia wakitaka kumpiga Dereva wagari ya aina ya Suzuki kuwa yeye ndio alisababisha ajali hiyo kwa kuyumbayumba kwake barabarani









WATU zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Costa kutoka Mbozi kuelekea Mbeya kupinduka katika eneo la  Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya.

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 336 CJY ambalo lilipinduka baada ya kumshinda dereva wakati akijaribu kulikwepa gari linguine aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 327 ARZ.

Kwa mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

Baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top