> Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri usidhani utatetemesha kila mwanaume | MAPENZI

Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri usidhani utatetemesha kila mwanaume

Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri na mrembo,usidhani utatetemesha kila Mwanaume, kuna wanaume na akili zao kichwani,urembo wako hauwasumbui kama bichwa lako ni kanyaboya,uzuri wako hausaidii kitu,na utashangaa no one is paying attention,watu utakaowapata ni walewale kanyaboya wenzako, na hawana futuretabaki unaliwa bure kila siku unatoa macho.

Ukipata mwanaume anakupenda unaanza drama zako na kupiga watu danadana,madai yako hujali na unadhani hata akiondoka utapata mwingine kisa wewe ni mzuri, la hasha Mwanaume akijitoa mhanga kukupenda kwa uzuri wako mheshimu,maana viumbe wa kike wakiwa wazuri ni shida na matatizo hakuna mtu anataka,sasa ukimwongezea na drama pamoja na yeye kujigeuza mpalestina kwako utajikuta umeolewa na kioo cha chumbani kwako,maana hicho ndo kinakudanganya sana kwamba we ni mrembo.

Watch out drama zina mwisho, leo unacheza na mioyo ya watu unajiona we kifaa usidhani wanaume hawaumii, tunaumia
sema hatusemi tu,machozi yetu kama ya samaki.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top