> Busu la kahaba lavunja ndoa kanisani...Cheki tukio zima hapa | MAPENZI

Busu la kahaba lavunja ndoa kanisani...Cheki tukio zima hapa



Hili nalo limeonekana kuchukua uzito mkubwa baada ya ndoa kuvunjika kanisani wakati mdogo wa kike wa bwana harusi alipoamua kwenda mbele na kumkiss kaka yake mbele ya bibi harusi kama ishara ya kuwapongeza.

Katika harusi hiyo ya kifahari iliyofanyika nchini India ilivunjika kwa ugomvi mkubwa miongoni mwa familia za pande zote mbili kufuatia tukio hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda kwenye harusi hiyo alisema dada huyo wa bwana harusi alifurahi sana kuona kaka yake anafunga pingu za maisha na kuamua kwenda kumpongeza.

Wapenzi hao ambao walikutana katika mtandao wa kijamii na kujikuta wakiingia kwenye mahusiano,waliamua kuhitimisha mapenzi hayo baada ya kupata baraka za wazazi na kuamua kuungana na kuwa kitu kimoja.

Baada ya tukio hilo familia ya bibi harusi walishikwa na hasira baada ya kuona mwanamke akimkis bwana harusi bila idhini ya mkewe huku akimvuta na kwenda kucheza naye mbele.

Katika harusi hiyo iliyohudhuriwa na watu zaidi ya mia tano,familia hizo hazikuishia hapo kwani waliamua kukunjana mashati huku mmoja wa viongozi wa mtaa Shakuntala Bharat akiwa shuhuda wa tukio hilo.

Baadaye familia ya bibi harusi iliamua kumshtaki bwana harusi na kuamua kumtupa jela kwa kumdhalilisha binti yao licha ya kuwa ni suala binafsi zaidi huku tukio hilo likiwashangaza wakazi wa eneo hilo kwani historia ya familia hizo inaonyesha wametoka katika familia zenye uwezo na zilizoelimika.

Badaye waliamua kuondoka bila ya bibi harusi huku kiongozi huyo akiwasaidia polisi waliofika eneo hilo kuwapa maelezo ya kilichotokea lakini moja ya familia hizo haikua tayari kutoa ushirikiano

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top