> Mapenzi...Mambo yanayochangia kupungua kwa hisia za mapenzi katika ndoa | MAPENZI

Mapenzi...Mambo yanayochangia kupungua kwa hisia za mapenzi katika ndoa

Ukweli ni kuwa watu wengi wanaodai hawatosheki katika mapenzi,ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi.Watu hao hawaangalii uwezo,nafasi,hisia na afya ya kukutana kimwili. Jambo muhimu analopaswa kuzingatia kila aliye kwenye uhusiano ni kwamba,kama unataka kutosheka na penzi la mpenzi wako,ni lazima utosheleze kwanza akili yako.Unapaswa kuamini kuwa uliyenaye ni bora na kwamba kama ziko kasoro,lililo la msingi ni kuzizungumza na kuziondoa.

Ukweli ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki mbali ya yale niliyotaja hapo juu,lakini pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao wa zanani,ambao labda walikuwa na uwezo mkubwa zaidi katika tendo kuliko akiye naye sasa.

Hata hivyo,wakati mwingine wanashindwa kuelewa kuwa hata wale wanaofikiri ni wazuri,kama wangekuwa nao hadi sasa huenda nao wasingeweza kuendelea kuwa imara.

Hii ni kwa sababu,watu wengi báada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu hupoteza nguvu au shauku ya tendo hilo.Zipo sababu nyingi za hali hiyo,mojawapo ni kutobadilika kwa mazingira au wapenzi kuanza kutoelewana kwa sababu mbalimbali kama vile kutojaliana na kadhalika.

NGUVU ZA KIJINSIA.
Kama hukuwa unafahanu,Ni kwamba idadi ya wanaume wasio na uwezo wa kufanya vyema tendo la ndoa inazidi kuongezeka.Tafiti zinabainisha kuwa wastani wa ndoa nne kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliwa na tatizo hiloPia wanaume sita kati ya 10 wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume,kwanba kama siyo kuwa na uwezo mdogo,basi hukosa kabisa nguvu za kuendelea.Wengine wanaweza kuanza,lakini hawawezi kuendelea na wengine hata kuanza ni shida.Idadi kubwa ya wanaume bado wanasumbuliwa na tatizo hili hasa kwa sababu ya kutokuwa tayari kuchukua hatua hasa za kuzingatia ushauri.
Ziko sababu nyingi za kukumbwa na hali hii,ikiwemo ulevi,kutofanya mazoezi,kujichua au utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta. Hata hivyo kwa kuzingatia tiba sahihi ya vyakula,mtu anaweza kupona.Kwa mfano kuna baadhi ya vyakula vikichanganywa kwa ustadi kama pilipili,parachichi na kadhalika vinaweza kunfanya mtu kuondokana na tatizo hilo.
Wengi wa watu walio kwenye ndoa za miaka mingi,wanafanya mapenzi kwa sababu tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja,lakini siyo kwa sababu ya kuwa na hisia kali.Matokeo yake ni wanandoa wengi kupata msisimko mdogo karika tendo la ndoa wanapokuwa na wenza wao. Hata hivyo,kwa kuzingatia utaalamu,wanaweza kuwa na furaha katika ndoa yao.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top