> Siri ya mapenzi ndo hii hapa...Uckubali ikupite (You must read) | MAPENZI

Siri ya mapenzi ndo hii hapa...Uckubali ikupite (You must read)

Hizi ni Njia 10 za kumfanya mpenzi asitoke nje Njia za kumfanya mpenzi asitoke nje

1. TAMBUA THAMANI YAKE Unapokuwa Umeapa Kuwa Utampenda Mwenzako Hadi Kifo Kitakapowatenganisha, Uwe Umefanya Hivyo Kwenye Nyumba Ya Ibada Au Kwingine, Lazima Ufahamu Jinsi Ya Kutambua Juhudi Za Mpenzi Au Mwenzi Wako, Ili Kuepukana Na Uwezekano Wa Mwenzi Wako Kukuona Kama Vile Unamchukulia Kawaida Na Hujali Jitihada Zake. Mtu Anapodhani Mwenzake Hajali Jitihada Zake Ni Rahisi Kushawishika Kutoka Na Kwenda Kwa Mtu Atakayeitambua Thamani Yake. Ili Kuondoa Uwezekano Wa Mwenzako Kudhani Humjali Wala Kuthamini Juhudi Zake, Mara Kwa Mara Jiulize Unaweza Kumfanyia Nini Ili Kumwonesha Kuwa Unamtambua. Jambo Lenyewe La Kumfanyia Linaweza Kuwa Rahisi Tu, Mathalani Kumtumia Ujumbe Mfupi Kwa Ajili Tu Ya Kumwambia Kuwa Yuko Mawazoni Mwako. Iwapo Utajenga Mazingira Ya Kuitambua Thamani Ya Mwenzako Mara Kwa Mara Haitakuwa Rahisi Kwa Mwenzako Huyo Kufikiria Kuchepuka.

2. JENGA UKARIBU NAYE Mara Nyingi Jamii Huwachukulia Wanaume Kama Watumwa Wa Ashiki Zao, Lakini Matukio Mengi Ya Kukosekana Kwa Uaminifu Hutokana Zaidi Na Mahusiano Ya Kikaribu Baina Ya Mwanamke Na Mwanamume Na Si Tamaa Ya Mwili Ya Mwanamume. Iwapo Wanawake Wote Wataufahamu Ukweli Huu, Watajua Jinsi Ya Kujenga Ukaribu Na Wanaume Zao Ili Kuwaondolea Uwezekano Wa Kutekwa Na Wanawake Wengine. Ni Kweli Kuwa Wapo Wanaume Wasioweza Kujenga Mshikamano Wa Kihisia Katika Suala La Mapenzi, Lakini Huku Bado Wakiendelea Kuvutika Kimwili. Jambo Kubwa Ambalo Mwanamke Anaweza Kulifanya Na Kumwepusha Mwanamume Kutoka Ni Kuhakikisha Ndiye Mtu Wake Wa Karibu, Huku Mara Kwa Mara Akiwa Ndiye Mwanzilishi Wa Wazo La Kufanya Mapenzi.

3. MSIKILIZE VEMA MWENZAKO Wanawake/Wasichana Huwa Na Mazoea Ya Kusemezana Na Marafiki Zao Mambo Mengi Ikiwa Ni Pamoja Na Siri. Hata Hivyo, Wanaume Huogopa Kuwashirikisha Wenzao Mambo Binafsi Ya Ndani. Ili Uweze Kuishi Vema Na Mwanamume, Lazima Ujue Jinsi Ya Kumhakikishia Mwanamume Kuendelea Kuwa Mwanamume Hata Unapomweleza Mambo Yaamshayo Mihemko. Kwako Wewe Mwanamke, Iwapo Utahisi Kuwa Mwanamume Wako Anataka Kuwa Wazi Katika Mambo Fulani Binafsi Lakini Anahisi Tu Kuwa Atapoteza Uanaume Wake Kwa Kueleza Mambo Yake, Mwekee Mazingira Ya Kumhakikishia Kuwa Ataendelea Kuwa Mwanamume. Msikilize Na Usimlaumu, Muulize Maswali Yanayohitaji Majibu Chanya. Utashangaa Jinsi Utakavyoboresha Ukaribu Wako Na Mwanamume Huyu Hivyo Kupunguza Uwezekano Wa Kukusaliti.

4. MWACHE AWE NA MARAFIKI Jambo Jingine Ambalo Linaweza Kumpunguzia Mwanamume Uwezekano Wa Kufanya Mapenzi Nje Ya Uhusiano Ni Kumhakikishia Urafiki Na Wanaume Wenzake. Kwa Vyovyote Vile, Lazima Mwanamume Wako Utakuwa Ulimkuta Na Marafiki. Usimzuie Kuendelea Kuwa Nao. Unapomuunga Mkono Mwanamume Katika Kampani Yake Na Wanaume Wenzake Utakuwa Umemwongezea Mwanamume Huyu Fursa Ya Kuendeleza Ukaribu Na Watu Wake, Hivyo Kupunguza Fursa Ya Kujipenyeza Kwa Wanawake Wengine Katika Maisha Yake. Ukimbanabana Halafu Na Wewe Ukashindwa Kuwa Rafiki Kwake, Akimpata Mwanamke Aliye Tayari Atashikamana Naye.

 5. TEKELEZA MALENGO NAYE Hata Kama Uhusiano Wako Na Mpenzi Wako Umedumu Tangu Mlipokuwa Vijana Wadogo Chuoni, Bado Haitoshi Kujihakikishia Kuwa Mmeshakua Pamoja. Ili Kuweza Kuepukana Na Uwezekano Wa Mwenzako Kukusaliti, Lazima Nyote Msaidiane Katika Kutekeleza Mambo Muhimu. Huku Ndiko Kukua Pamoja. Njia Rahisi Zaidi Ya Kukua Pamoja Na Mpenzi Wako Au Mwenzi Wako Wa Maisha Ni Kuweka Malengo Na Kuyatekeleza Kwa Pamoja. Mfano, Kama Mmeishi Katika Nyumba Ile Ile Kwa Miaka Kadhaa Na Mazingira Yamewachosha (Pengine Nyumba Yenyewe Ni Ya Kupanga), Pendekeza Kuhamia Sehemu Nyingine — Unaweza Kukuta Hata Mwenzako Kumbe Ana Hisia Kama Hizo. Iwapo Utazigusa Hisia Zake Kwa Pendekezo Lako, Mpenzi Wako Atajihisi Kuonekana Wa Tofauti Machoni Pako. Na Kwa Kuwa Baadhi Ya Watu Wanaotoka Nje Ya Ndoa Huenda Kutafuta Utofauti, Utakuwa Umemzuia.

6. JITAHIDI KUMWELEWA Mojawapo Ya Vishawishi Vikuu Vya Mwanamume Kujiingiza Katika Mapenzi Ni Kumpata Mtu Ambaye Atamwelewa. Kama Huna Sifa Hii, Ni Rahisi Kwa Mwanamume Wako Kutoka Kwa Ajili Ya Kuitafuta Kwingine. Ili Kumzuia Mwanamume Kutoka, Onesha Jitihada Za Kutaka Kumwelewa Na Kufahamu Matakwa Yake Ili Uweze Kuyatimiza. Katika Hili Usiogope Kumuuliza Maswali Magumu, Mathalani Waweza Kumuuliza “Unajisikiaje Kuhusiana Na Uhusiano Wetu?” Au “Ni Kitu Gani Ulichokuwa Unakitaka Katika Uhusiano/Ndoa Ambacho Hujakipata Mpaka Sasa?” Namna Hii Utakuwa Umeonesha Jitihada Za Kutaka Kumfahamu Na Kumridhisha.

7. SISITIZA ZAIDI MATENDO Wanawake Wana Utamaduni Wa Kupenda Kuyazungumza Mambo Yao, Ikiwa Ni Pamoja Na Matatizo. Hili Ni Jambo Jema, Isipokuwa Tu Kinachotakiwa Ni Kuweka Uwiano Kati Ya Maneno Na Matendo. Mwanamke Hapaswi Kujiondoa Katika Hulka Yake Asilia Ya Kupenda Kusema Ili Aweze Kudumisha Uhusiano Wake Na Mwanamume, Lakini Mara Kwa Mara Ni Vema Badala Ya Kusema Tu Ukafanya Shughuli Kama Mbadala Wa Kusema. Badala Ya Kusema Sana, Unaweza Kumshirikisha Mwanamume Katika Shughuli Fulani Ambayo Nyote Mnaipenda, Jambo Ambalo Litaonesha Umoja Wenu, Huku Kila Mmoja Akipata Jibu Kwa Nini Alichagua Kuishi Na Mwenzake. Mathalani, Badala Ya Kuzungumzia Jinsi Usivyojisikia Vema Kwa Namna Msivyopata Muda Mwingi Wa Kuwa Pamoja Na Kuzungumza, Tumia Fursa Hiyo Kuzungumza Kile Ambacho Umekuwa Ukitaka Kuzungumza Na Mpenzi Wako, Maana Sasa Yupo. Badala Ya Kuzungumzia Jinsi Unavyopenda Kujifunza Mapishi Fulani, Chukua Hatua Ya Kwenda Kujifunza, Na Ikibidi Uende Na Mwenzako. Namna Hii Utaonekana Zaidi Kama Mtu Ambaye Unatenda Maneno Yako, Si Kuzungumza Tu. Kwa Jinsi Hii Mpenzi Wako Atavutika Kwako Zaidi.

8. USIMWONDOLEE UJINSIA WAKE Watu Wengi Katika Makuzi Yao Huwa Na Dhana Kuhusiana Na Jinsi Mwanamume Au Mwanamke Anavyopaswa Kuwa. Kwa Mwanamume, Wengi Huamini Kuwa Atakuwa Mtendaji Kuliko Msemaji, Asiyetawaliwa Na Mihemko, Mtawala, Jasiri, Hodari Na Kadhalika. Lakini Katika Kipindi Cha Takriban Miongo Mitano Iliyopita, Hadhi Na Hulka Za Wanaume Na Wanawake Zimebadilika. Isipokuwa, Bado Wanaume Halisi Wameendelea Kuwa Wanaume, Kama Ambavyo Wanawake Halisi Wameendelea Kuwa Wanawake. Iwapo Utakuwa Na Mazoea Ya Kumlazimisha Mwanamume Wako Kufanya Mambo Ambayo Si Ya Kianaume, Au Ambayo Hayadhanii Kuwa Ya Kianaume, Mwanamume Huyu Anaweza Kulazimika Kwenda Kumtafuta Mwanamke Ambaye Anampa Fursa Ya Kuendelea Kuwa Mwanamume. Ili Kuondoa Uwezekano Wa Mwanamume Kutafuta Mahala Ambapo Uanaume Wake Utatambuliwa, Jaribu Kufikiria Mambo Ambayo Humfanya Mwanamume Kujihisi Kuwa Mwanamume Kweli. Namna Hiyo Utaongeza Mapenzi Yake Kwako.

9. PUNGUZA TAHADHARI Mojawapo Ya Mambo Ambayo Huzuia Mahusiano Kufikia Ukamilifu Wake Ni Watu Kuishi Kwa Tahadhari Wakiogopa Kuingia Katika Maeneo Ambayo Yanaweza Kuondoa Furaha Yao, Pengine Kwa Mmoja Wa Wenza Hao Kukwazika. Ni Kweli Kuna Umuhimu Wa Kuepuka Kumkwaza Mwenzako, Lakini Mnapoishi Kwa Tahadhari Kubwa Ni Vigumu Kufikia Ukamilifu Wa Uhusiano Wenu Na Ni Rahisi Kwa Mwenza Kutoka Kwa Ajili Ya Kupata Uhuru Na Amani Zaidi. Ili Kuepusha Balaa, Jiulize Ni Wapi Wewe Na Mwenzako Hamkubaliani. Ukishayapata Mambo Ambayo Hamkubaliani, Jaribu Kuweka Uwiano Na Kumpa Uhuru Mwenzako Katika Kuyafanya Hayo. Namna Hii Utaongeza Ukamilifu Katika Uhusiano Wenu Na Hisia Za Kubanwa Zitaondoka.

10. JISHUGHULISHE AKUKOSE Wanawake Hupenda Zaidi Vitu Ambavyo Ni Haba Au Hupatikana Kwa Nadra. Katika Uhusiano Wa Kimapenzi Mwanamke Hatakwambia Kuwa Anataka Uondoke Ili Aweze Kupata Fursa Ya Kukumisi Na Kutamani Kukuona, Lakini Ukweli Ni Kwamba Ukipatikana Kwa Nadra Utaongeza Mvuto Wako Kwake, Ilimradi Tu Uwe Na Sababu Ya Kupatikana Kwa Nadra. Lazima Ujue Jinsi Ya Kumfanya Mpenzi Wako Akuhitaji. Jishughulishe Na Uchakarike, Kwani Kwa Kufanya Hivyo Utaongeza Kipato Chako Na Kumwongezea Usalama Na Uhakika Mpenzi Wako, Lakini Pia Utampa Mpenzi Wako Fursa Ya Kukumisi Na Kupunguza Uwezekano Wa Kukusaliti.

MSHIKE MWENZIO Huwezi Kumzuia Mpenzi Wako Kutoka Na Wanaume/Wanawake Wengine Kwa Kuwa Na Wivu Na Kumfuatiliafuatilia. Lakini Kwa Kuzingatia Mambo Haya Yaliyobainishwa Hapa, Utakuwa Umeondoa Sababu Nyingi Za Mpenzi Wako Kufikiria Kuwa Na Uhusiano Na Mtu Wa Nje.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top