> Mapenzi yatakuliza mpaka lini soma hapa Ujue jinsi ya kuyahepuka makosa yakukuliza.. | MAPENZI

Mapenzi yatakuliza mpaka lini soma hapa Ujue jinsi ya kuyahepuka makosa yakukuliza..

Ni vijimambo tu vya ‘malove dave’, si unajua bila mapenzi maisha yanakuwa na
mushkeli? Bila shaka jibu ni ndiyo na huo ndiyo ukweli, binadamu hawezi kuishi
kama jiwe, mti au amoeba.

Raha ya maisha ni kuwa na mwenzi wa kumpenda na kukupenda kiukweli wala siyo
kuzugana. Hayakuumbwa mapenzi bila sisi, na hiyo ndiyo sababu ya kutangulia
Adam na Hawa kisha yenyewe yakafuata katikati yao.

Kwa wale walio katika mapenzi matamu na ya kweli watakubaliana na mimi kuwa pale penye amani ni kama paradiso ndogo ndani ya ulimwengu huu mkubwa uliojaa vituko!
Si ajabu kujikuta umeshiba bila kula, eti kwa sababu tu umemuona mpenzio au kuwa
naye karibu. Yeye si ndiye mambo yote, kwahiyo kuna haja gani ya kujaza tumbo
kwa sembe wakati sura na harufu yake vinakushibisha? Raha iliyoje!
Wakati watu wengine wakiishi kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wanaoteseka
huku mioyo yao ikiwa imesinyaa! Kila
siku ni karaha na vituko vya makusudi.
Japo wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote, lakini wanatendwa. Kila siku mioyo imejikunja kwa simanzi inayotokana
na maumivu yasiyojulikana mwisho wake.

Kisa kupenda!
Lakini pamoja na karaha, vituko na dharau bado kuna wale wenzangu na mimi utakaowasikia wakisema; “Ah! Nitavumilia tu, labda atabadilika na nafikiri
sitoweza kumuacha kwa kuwa nampenda sana!”
Hey! Shtuka ndugu yangu, labda pengine mimi nikawa na msimamo tofauti kidogo.
Ninavyoamini ni kwamba mapenzi ya kweli ni pamoja na kumsikiliza mwenzako na
kuheshimu hisia zake.
Tofauti na hapo, tabia ya kutokuwa msikivu, kutojali na kutokuwa mwepesi kubadilika ni dalili tosha ya kutokuwepo kwa upendo wa dhati. Mapenzi ni kupenda, kupendwa,
kusikilizana na kuheshimiana na si zaidi au chini ya hapo!
Kama unamkemea kuhusu tabia yake ya kurudi nyumbani usiku na hataki kubadilika, unangoja nini tena? Hapa naomba niwape pole wale wote wanaokwazwa na wapenzi
wao kwa namna moja au nyingine.

ANGALIZO; Kama mpenzi wako anakuumiza kutokana na ulevi wake, ujeuri, kutojali, ubabe na mengineyo mengi, huo ni mtihani mzito!
Pamoja na hivyo, nafahamu kuwa wakati mwingine ni vigumu kuamua hatma ya uhusiano wako
kwakuwa unahisi unampenda sana na hauko tayari kumkosa maishani. Dondoo
zifuatazo zitakusaidia;
 Zingatia thamani kubwa ya chozi lako!
Nadhani nitakuwa wa ajabu kama nitaanza kuchambua muktadha wetu wa leo bila kutanguliza shukurani zangu kwa Mungu mpaji wa viumbe vyote. Unadhani jeuri hiyo nitaipata wapi, ikiwa kila ninachofanya si kwa ujanja wangu, bali ni kwa matakwa yake?

Si mimi tu, hata wewe ni wajibu wako kumshukuru kwa mema yote anayokutendea kila siku, hivyo tuungane pamoja katika kuzienzi kudura zake, tukiamini kwamba kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kutusafisha mbele yake.
Mada yetu inayouliza “Utalia mpaka lini kisa mapenzi?” Bado inaendelea na leo tupo sehemu ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho. Lengo ni kukuzindua ili uzingatie kwamba thamani ya chozi lako ni kubwa, hivyo haupaswi kumtolea mtu ambaye hakuthamini.

Katika matoleo mawili yaliyopita, niliandika kuwa kuna mambo ambayo unaweza kuyaacha yapite kwa kigezo cha kujiongopea kwamba unavumilia, na hayo ndiyo hasa yanaweza kukufanya udhalilike. Ni nani atakayekuheshimu ikiwa unashindwa kujilinda?
Niliandika kuwa mapenzi ni kupenda, kupendwa, kusikilizana na kuheshimiana wala siyo zaidi ama chini ya hapo! Tofauti na hapo, tabia ya kutokuwa msikivu, kutojali na kutokuwa mwepesi kubadilika ni dalili tosha ya kutokuwepo kwa upendo wa dhati.
Tunashauriwa kuwa wavumilivu, lakini siyo katika kipimo cha kutufanya tudharauliwe. Miongoni mwetu tupo tunaojifanya ni wastahimilivu mpaka kufikia katika levo ambayo pengine inamkasirisha hata Mungu. Leo unamfumania, kesho upo naye, unangoja nini?

Karaha, vituko na dharau ni chungu tele, lakini wenzangu na mimi utawasikia wakisema “Ah! Nitavumilia tu, labda atabadilika na nafikiri sitoweza kumuacha kwa kuwa nampenda sana!” He! Mpaka lini na dunia iliyochafuka hii?
Pamoja na hivyo, nafahamu kuwa wakati mwingine ni vigumu kuamua hatma ya uhusiano wako kwakuwa unahisi unampenda sana na hauko tayari kumkosa maishani. Ndiyo maana ya kukupa dondoo zifuatazo ili zikusaidie…

ZINGATIA BUSARA ZA WENGINE
Matukio ni mengi mpaka yanakatisha tamaa, hivyo wakati mwingine ni vema sana ukawaona watu ambao unaamini akili zao ‘zimeseto’, na kuomba ushauri. Busara zao zitakusaidia cha kufanya pindi unapokabiliwa na msongo wa mawazo unaotokana na kero za mpenzi wako.
Kwa wanandoa wanaweza kuwahusisha wazee au vyombo vya sheria. Usikubali “kumezea” matatizo uliyo nayo, utakufa kihoro bure! Waombe ushauri wale unaowaamini. Bila shaka watakuonesha njia!

SOMA KWA MIFANO
Matatizo ni sehemu ya kila binadamu, na linapokuja suala la kutatua yetu wenyewe ni vizuri kusoma kwa wengine, ni kwa namna gani walipopatwa na matatizo kama yetu walivyojiokoa.
Hili halina ‘ujiniaz’, haujawahi kusikia kinyozi hajinyoi? Jiulize, ni wangapi unaowafahamu au kusikia habari zao, waliowahi kupenda kama wewe lakini kutokana na manyanyaso, wakaachia ngazi?
Jiulize tena, baada ya hao waliopenda tena pengine kuliko wewe, walipoachana na wenzi wao walikufa au kupata ugonjwa wowote wa kudumu? Jibu, hapana tena pengine wanaishi maisha mengine matamu na wapenzi wapya. Kama wao wameweza wewe unashindwa nini?

AMINI KUWA MAISHA YAPO BILA YEYE
Ulipozaliwa haukuwa na fikra kwamba utakutana naye na kuunda umoja utakaowaingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi. Kama zilivyo safari za watu wengine katika maisha, ukakutana naye na kuamini mtakuwa pamoja daima.

Baadaye, unakuja kusadiki msemo kuwa ‘kunguru hafugiki’, sasa baada ya kulijua hilo, unangoja nini? Amini kuwa maisha yapo hata bila yeye, achana na mawazo kuwa hauwezi kuishi bila yeye.
Ukiamini hakuna maisha bila huyo mpenzi wako anayekutesa, inakuwa ni sawa na kujifunga minyororo na kufuli nzito. Hebu jaribu kupigana kiume na kama ni mwanamke kataa kunyanyaswa, hakuna binadamu anayeshikilia pumzi ya mwingine.

NI VIZURI UJIAMINI
Suala la mapenzi ni hisia ambazo ni zoa la moyo, hivyo kusema ule ukweli, suala la kuamua kumuacha unayempenda kwa dhati siyo dogo. Linaumiza na kwa wale wenye tabia ya kurudisha taswira ya matukio nyuma, huwatoa machozi mengi.
Hata hivyo, hufikia hatua ya ‘point of no return’ kwamba sasa imetosha, nakwenda sirudi nyuma. Katika hatua hii huhitaji mtu mwenye kujiamini na jasiri kwelikweli ili kuondokana na maisha ya “roho juu” kila siku! Potelea mbali, acha penzi la balaa liondoke na kukaribisha uhuru wa nafsi.

KUWA NA MATARAJIO CHANYA!
Jitihada hazishindi kudura, ndiyo maana tunaweza kutumia fedha, akili na nguvu kuwafanya wenzi wetu watulie ili kujenga uhusiano wenye afya, lakini ikashindikana.
Kwa mantiki hiyo, ni vizuri utambue kuwa huenda Mungu hakukupangia ufurahie maisha na huyo uliye naye sasa kwa sababu yule wako “orijino” bado yupo njiani na akifika atakusahaulisha shida zote. Hiyo ndiyo sababu ya kukutaka uwe na matarajio chanya.
Yes, kama anakutesa achana naye, wako anakuja.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top