> Mazingira 10 yanayopia uaminifu na upendo wa kweli katika Mapenzi.. | MAPENZI

Mazingira 10 yanayopia uaminifu na upendo wa kweli katika Mapenzi..

Mambo yanayoweza kujaribu uaminifu wako
1. Magonjwa/Maradhi
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata wakati akiwa na magonjwa na maradhi?

2. Kukosa watoto
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata kama itaonekana amechelewa au hana kabisa uwezo wa kuzaa mtoto au hana nguvu za kuweza kukuzalishia motto?

3. Uzazi
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata kipindi cha uzazi? Hasa kwa wanaume. Kuna wakati mke anakuwa na “complication” za uzazi na inamchukua muda mrefu sana kupona au kurudi katika hali yake ya kawaida. Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda na kutunza patano lenu?


4. Maendeleo ya ghafla
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata pale ambapo umepata fedha na mali nyingi kwa ghafla bila kutegemea? Au ndio utamuona ni mshamba, hajasoma, hajui kwenda na wakati na kumtoa kasoro kibao kwasababu sasa umefanikiwa kifedha na kimaendeleo? Ukasahau ulikotoka naye.

5. Kukosa kazi
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata kama itatokea amepoteza kazi na kwamba hakuna anachozalisha tena na badala yake anakutegemea wewe kwa kila kitu? Utaendelea kumuona ni mwenzi wako kipenzi, Dear, honey, sweethear, baby, au ndio utamuona kama amekuwa mzigo usiobebeka?

6. Kutengana kwa muda mrefu
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata inapotokea kwamba mmetengana kwa sababu za kimazingira? Labda amefungwa jela, amekwenda masomoni kwa muda mrefu, amehamishwa kikazi kwenda mbali usipoweza kumfikia nk. Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda na kumsubiria?

7. Uzee
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata kama anaonekana sasa amekuwa mzee tofauti na kipindi mlipoonana? Utaendelea kumpenda kama alivyo au ndio utaanza kutafuta dogodogo ambao wanaonekana wabichi?

8. Umasikini
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata kama amekuwa masikini au anaishi maisha ya kimaskini? Au ndio utamtupa na kutafuta wale waenye nazo?

9. Kutoweza kufanya tendo la ndoa
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata wakati itaonekana amepotez auwezo wa kushiriki tendo la ndoa? Utaendelea kumpenda na kumthamani au ndio utatafuta njia mbadala?

10. Kushindwa Kutimiza Makubaliano
Utaendelea kuwa mwaminifu na kumpenda mwenzi wako hata kama itatokea ameshindwa kutimiza baadhi ya vigezo na makubaliano mliyojiwekea

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top