> Nimemfumania mpenzi wangu na mwanamke mwingine..Ametubu anataka turudiane nifanyeje???? | MAPENZI

Nimemfumania mpenzi wangu na mwanamke mwingine..Ametubu anataka turudiane nifanyeje????

Watanzania wenzangu naombeni mnisaidie mwenzenu, Katika maisha yangu yote hadi sasa nina miaka 24, sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine, zaidi ya huyu mchumba wangu nilie nae, nampenda kuliko kitu chochote

Tumeanza urafiki wetu nikiwa na miaka 21 ila mchumba wangu amebadirika sana, alisema atanioa, amejitambulisha na kwetu, lakini gafla, ameahirisha, anasema kwa sasa mambo yamekuwa mengi sana, na hata maongezi yake si ya kawaida, yani anaongea as if amekasirika, sasa ile hali mimi siipendi, kila nikijaribu kupeleleza ili nijuwe labda nimemkosea, sipati jawabu lolote,
Baada ya kuchunguza sana, nikagundua anatembea na secretary wao, na ninasikia tu kwa watu kuwa anataka kumchumbia, nimelia sana na moyo wangu wala hautaki kuamini hili, nilishawahi taka kunywa vidonge nife, dada alinikuta, na kunisema sana, lakini bado akili haijakaa sawa,

Mwezi uliopita rafiki wa mchumba wangu, alikuja yeye na dada yake, wakaomba kuongea na mimi, I thought kwamba wametumwa na Rick (mchumba wangu), kumbe walikuja kwa mengine,

Kilichomleta ni kwamba, anataka kunioa yeye, anadai alikuwa akiichunguza tabia yangu toka siku nyingi na kudai kuwa mchumba wangu si mwaminifu, lakini kwakuwa hatujafunga ndoa, basi yeye anataka kunioa, na dada yake ni mtumzima amethibitisha hilo, mimi nilikataa kata kata, nikawafukuza kwa hasira,

Nilimpigia sim mchumba wangu kumwambia, alichukia sana, akachukuwa company yake, wakalewa wakaenda kumpiga, walimpiga sana, Yule kaka alinitumia sms hii, ‘’ iko siku utanikumbuka’’ dada, sikuamini siku ambayo nilitoka safari, na kupitiliza kwa mchumba wangu nikamkuta na yule secretary wao, nilikwenda moja kwamoja kwakuwa sikumpata kwenye simu kumjulisha kuwa nakwenda. Na ni wiki ile ile ambayo rafiki yake alipigwa,

Toka siku ile moyo wangu umekufa ganzi nilimchukia gafla na nikaona siwezi kuishi bila yeye. alipoitwa na baadhi ya jamaa zangu, alisema kuwa nibahati mbaya tu shetani alimpitia! Ila Bado ananipenda, na anataka anitolee mahari kabisa ili tufunge ndoa, lakini dada yangu ananikatalia maana ndie alienilea toka mdogo. Sasa nishaurini mdogo wenu nifanyaje? Sijielewi, nimsamehe, au nimkubali Yule rafiki yake

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top