> Uwezo wa mwanamke kumsaidia mpenzi wake mwenye upungufu wa nguvu za kiume ni... | MAPENZI

Uwezo wa mwanamke kumsaidia mpenzi wake mwenye upungufu wa nguvu za kiume ni...



Leo nitaongelea mada kali kidogo ambayo inawakuta wanandoa wengi lakini wanaishia kunyamaza kwani hawana pa kusemea.

Kuna baadhi ya akina mama wanalalamika na wengine wanadiriki kutoka nje ya ndoa, ukiuliza kwa nini wanajibu eti mume hana ‘nguvu za umeme’ yaani za kiume.

Niwaambie, mnakosea, mwanamke uliyeamua kuwa na mume kwa shida na raha unatakiwa kumsaidia hata linapotokea tatizo kama hilo, kubwa si kumkimbia kama wafanyavyo watu wengine.

Hapa siongelei wale wenye tabia za kishoga, naongelea wale wanaume wanaoishiwa nguvu wakati wakiw katika tendo kutokana na kuwa na ugonjwa kama vile wa kisukari, vidonda vya tumbo, figo kufeli na msongo wa mawazo.
Unajua kwa wenye tatizo la kishoga naweza kusema kuwa Mungu si mjinga kuwaumba hivyo. Wapo wanaojibadili na kuwa wanawake eti ukiwauliza wanasema wana homoni nyingi za kike!

Mimi leo naongelea wale wanaume marijali waliopatwa na magonjwa niliyoyataja.

Baadhi ya wanawake hawana uelewa kabisa, akimuona mumewe hawezi basi anaanza kumwambia kuwa amemsaliti kwa kutoka nje ya ndoa yao.
Kwa nini msikae chini na kuongea naye taratibu mkagundua tatizo na mkakubaliana cha kufanya.

Njia unayoweza kuitumia mwanamke mwenzangu ni kuhakikisha unamshika mkono mumeo na kumuuliza nini ukimfanyia atafanikiwa kupata nguvu za umeme na injini ikawaka kama zamani na kufurahia ndoa yenu badala ya kumnunia na kumpa mgongo.

Kwa upande wa wanaume ambao tayari mna matatizo hayo msijione wanyonge.
Mwanaume unaweza kumsaidia mkeo kwa njia nyingi tu kwa kumridhisha huku ukimpa maneno mazuri hata asifikikirie kutoka nje ya ndoa yenu na kwenda kukutia aibu.

Ukumbuke ukilifumbia macho hili mjomba, jirani , hata wakwe watakujua kuwa huna umeme kwa sababu mwisho wa siku mkikaa kikao cha kwa nini mkeo anakusaliti ataitoa siri yako na itakuumiza maisha yako yote wakati imetokea bahata mbaya kupatwa na maradhi hayo.

Mwanamke mwenzangu, mumeo anaweza kukwambia  anataka mahaba, usimkatalie kamwe hapo ndiyo anaweza kukusaidia wewe na yeye ikawa ni faraja yake. Mwachie mwili bibi kwani ameutolea mahari kwa ajili ya kufaidi, kwa nini umbanie na kumkatalia?

Mwisho nawasihi wanawake wenzangu msitoke nje ya ndoa kwani wanaofanya hivyo siku zote wanadharaulika sana na kwa Mungu utaulizwa siku moja sababu ya kumtesa mumeo. Kumbuka kuna radhi ya mume ambayo ikikushika ni mbaya sana.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top