Mwanaume mtakatifu ni yule anaemwachia maamuzi yote mwanamke, anaona
kuonyesha upendo wa hali ya juu ndo kutamfanya mwanamke akae na
kupendezwa na yeye zaidi.
Mwanamke anapenda mwanaume
kiongozi, anayejiamini na kujua jinsi ya kujisimamia. Ninajua hili
litakushangaza, Mwanamke anapenda kupewa vikwazo na kuchemshwa akili,
maana kunamfanya awe anakufikiria zaidi na kukutaka kukujua na
kukubadilisha hii inamfanya hamasa yake juu yako kuongezeka na kuvutiwa
na wewe zaidi, iwapo akikuzoea na kukuona wa kawaida na kukukariri kila
kitu unachofanya hamasa zake hupungua na kukuona kama unaboa maana
kunakua hamna kitu kinachomshangaza kuhusu wewe na hapo ndipo nguvu ya
mahusiano hubadilika na kumfanya yeye kuwa na sauti ndani ya mahusiano
na kukuona kama hauna kiwango cha kuwa mwanaume wake.
Hivi
ni vitu vinavyoweza kufanya uonekane mwanaume mtakatifu na
kukusababishia kupungua kwa nafasi ya kumpata mwanamke umtakaye na kama
tayari unae basi wewe unakua hauna nguvu kwenye mahusiano na kumfanya
mwanamke kukuendesha kama gari bovu.
1, Unamkubalia kwa kila kitu anachotaka.
Msimamo
na kujiamini ni kitu ambacho ndicho hukutengenezea heshima kwa
mwanamke, unatakiwa uonyeshe uanaume wako, akikwambia kitu kiangalie kwa
marefu na mapana na toa jibu kulingana na uonavyo na si kukubaliana nae
kwa kila kitu, hii itamuonyesha jinsi ulivyo mwanaume kiongozi na iwapo
ukianzisha familia nae atakua na imani nawe kuongoza familia, iwapo
ukimkubalia kwa kila kitu anachotaka atakuona si mwanaume halisi na
kukudharau maana utaharibu maisha yake.
2, Unahisia kupitiliza, unamuhitaji kuliko.
Kila
kitu kinanafasi, ukikizidisha hauwezi kuuona uzuri wake tena. Hata
mapenzi nayo yanahitaji nafasi, ukimuhitaji mwanamke muda wote unataka
kuwa nae mapenzi hayawezi kunoga zaidi, atakosa hata muda wa kukumisi na
kusababisha hamasa zake kushuka sababu ya kukuzoea na kukuona wa
kawaida, na hata kama ulikua ndo unamtongoza ataishia kukuchukulia kama
rafiki tu.
3, Unaomba msamaha kwa kila kitu.Kila kitu si cha kuomba msamaha, ukiwa unaomba msamaha kwa kila kitu unakua unapoteza thamani ya neno na kumfanya msichana asijisikie vizuri na kukuona wa ajabu na unakua unajishushia heshima yako kwa ujumla.
3, Unaomba msamaha kwa kila kitu.Kila kitu si cha kuomba msamaha, ukiwa unaomba msamaha kwa kila kitu unakua unapoteza thamani ya neno na kumfanya msichana asijisikie vizuri na kukuona wa ajabu na unakua unajishushia heshima yako kwa ujumla.
4,
Unaaibu kupindukia.Aibu mara nyingi inatokana na kutojiamini na kutojua
thamani yako, kitu cha kwanza mwanamke anachopenda kukiona kwa mwanaume
ni jinsi anavyojiamini, aibu itakufanya thamani yako ipungue kwake na
hata kama alikua amependezwa na wewe basi hamasa itaanza kupungua.
5, Unamsubiri kwa kila kitu mpaka aanze yeye.
Mwanaume
kwa mwanamke ni kiongozi, iwapo utashindwa kuwa na msukumo wa kuanzisha
mambo atakuona kama ni mtu usiejua jinsi ya kujisimamia na wala huwezi
kufanya kitu chochote cha maendeleo na itasababisha akudharau kwa hilo
na utapoteza sifa ya kuwa nae.
6, Hauwi mbunifu.Mapenzi
yanahitaji ubunifu, na kama mwanaume unatakiwa kuwa mbunifu wa
kubadilisha mambo na mazingira ili kumuongezea hamasa juu yako, jua
jinsi ya kumfanya atabasamu ambapo amenuna, na kumfanya avutike zaidi na
kupendezwa zaidi na wewe, usipokua mbunifu na kufanya mambo yale yale
utamboa na atakuona wa kawaida na kufanya hamasa yake kupungua na ndivyo
na thamani yako itakua inaisha.
7, Huonyeshi mipaka yako na hausemi hapana.
Kila
mtu anamipaka yake, iwapo amekuudhi hakikisha unafanya kitu
kitakachomfahamisha amevuka mipaka, kama kuna kitu kmekukera sema
hapana, onyesha unavyojiamini na usionekane bwege na kukufanya
akudharau, kama kitu hakiendani nawe onyesha, hii itatengeneza heshima
na kufanya avutike na wewe zaidi, tofauti na hapa ukiwa ni mtu wa
kucheka cheka tu lazima akudharau.
8, Unaona heri akuumize moyo kuliko kuachana nae.
Kung'ang'aniza
mapenzi ni kitu kibaya sana, kunamfanya mwenza wako akudharau na
kukuondoa kabisa moyoni, na hata kama kulikua na hamasa ndogo imebaki
basi lazima ipotee, jua mipaka yako na kama mapenzi yamefika mwisho jua
muda wa kuondoka.
9, Unatumia muda mwingi na yeye pamoja na marafiki zake.Marafiki wake wakikuzoea sana, dharau huanza maana utakua mtu wa kawaida tu, na marafiki zake wakishakudharau ujue huna nafasi tena.
9, Unatumia muda mwingi na yeye pamoja na marafiki zake.Marafiki wake wakikuzoea sana, dharau huanza maana utakua mtu wa kawaida tu, na marafiki zake wakishakudharau ujue huna nafasi tena.
10, Unamnunulia zawadi kila muda bila sababu na kutoa sifa pale zisipohitajika.
Zawadi
ikizoeleka inapoteza uzito wake na sifa nazo vivyo hivyo zikiongewa
sana zinakua hazina mvuto tena zaidi ya kushusha hamasa yake na kukuona
wewe ni wa mzaha.
Post a Comment