> Mambo yanayosababisha kupungua kwa hisia za mapenzi katika mahusiano | MAPENZI

Mambo yanayosababisha kupungua kwa hisia za mapenzi katika mahusiano

Mambo yanayochangia kupungua kwa upendo katika Mahusiano ya kimapenzi yapomengi mno..Ila leo tutajaribu tu kuangalia baadhi ya mambo makuu mawili ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha kupunguza upendo kwa wapenzi wengi..
>>Kutokumkubali mpenzi wako jinsi alivyo
Hapa namaanisha kuwa wapenzi wanabidi wakubaliane/washirikiane katika shida na raha na kama haitakuwa hivyo basi itakuwa sababu kubwa yapungua kwa mapenzi, walio wengi katika mahusiano siku zote hutegemea faida tu hasa za kifedha, unaweza kumkuta mtu anampenda mpenzi wake pindi awapo na hela na kama ikitokea siku mpenzi wake kakosa hela na zikikosekana basi hapakaliki na mapenzi hakuna na hapa ndipo watu wanasahau kuwa mapenzi si pesa bali ni hisia zilizopo ndani ya watu wawili hivyo basi kusiwe na vikwazo ambavyo havina mantiki. kubaliana na hali halisi ikitokea unashida ya pesa au kitu chochote toka kwa mpenzi wako muombe kama anacho atakupa au kukununulia na kama hana atakuambia. 

>>Kugombana kila wakati
NI kweli mapenzi bila kugombana kidogo hayahendi au pengine mtakuwa wanafiki ila si mpaka mnakosa amani katika mahusiano yenu na ikisha fikia hapo basi jua kuwa upendo lazima utapungua tu Mfano:-Ikitokea katika mahusiano wapenzi hawapatani na kila mmoja wao hataki kukubali kosa wote wanajiona wapo sahihi halafu mwisho wa siku wanapatana ghafla bila kuombana msamaha ni wazi kabisa kosa bado litakuwa halijarekebishwa hivyo ni rahisi kutokea tena ugomvi na ikitokea kila siku penzi lenu linatawaliwa na ugomvi nirahisi penzi lenu kupoteza muelekeo, kujikuta upendo unapungua na fikra za kutaka kumtafuta mpenzi mwingine.

Kwale inatosha tukutane tena katika mada nyingine.....Asante kwa kuwa pamoja nami

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MAPENZI Published.. .
Back To Top